• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Kagame Cup 2018: JKU yashinda jana, leo ni APR kupimana na Simba

  (GMT+08:00) 2018-07-02 10:51:08

  Katika mechi zilizopigwa jana mjini Dar es Salaam, Timu ya JKU kutoka Zanzibar imepata ushindi wa magoli 2-0 ilipocheza dhidi Kator FC ya Sudan Kusini, kwa magoli yaliyofungwa na Nassor Matar pamoja na Mussa Abrahaman.

  Mechi nyingine ilikuwa kati ya Gor Mahia ya Kenya dhidi ya Rayon Sport kutoka Rwanda, na timu hizo zilitoka sare ya magoli 2-2, kukishuhudiwa Rayon wakifanikiwa kusawazisha magoli yote mawili baada ya Gor kutangulia.

  Nayo Azam FC ya Tanzania ilitoshana nguvu na Vipers FC kutoka Uganda kwa sare ya magoli 1-1, na hii ikiwa ni baada ya nyota wa Vipers Daniel Sserunkumma kufunga goli la kusawazisha baada ya Azam kutangulia kwa goli lililofungwa mapema na Shaban Idd.

  Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi mbili, ambapo Singida United ya Tanzania inacheza dhidi ya Dakadaha FC ya Somalia, nayo Simba ya Tanzania itakuwa kibaruani dhidi ya APR kutoka Rwanda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako