• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raga, Kufuzu kombe la dunia: Kenya yaishinda Zimbabwe, sasa kucheza na Uganda jumamosi

    (GMT+08:00) 2018-07-02 10:52:04

    Baada ya kupata ushindi wa alama 45-36 dhidi ya Zimbabwe kwenye mechi ya kufuzu kombe la dunia kwa mwaka 2019 iliyofanyika siku ya jumamosi iliyopita mjini Nairobi, timu ya taifa ya Kenya inatarajiwa kucheza mechi nyingine jumamosi ijayo dhidi ya Uganda.

    Ushindi iliopata dhidi ya Zimbabwe uliifanya Kenya iendelee kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi la kufuzu nyuma ya Namibia.

    Jumamosi ijayo, nayo Zimbabwe ambayo inashika nafasi ya tatu sasa inatarajiwa kucheza dhidi ya Tunisia, na Namibia itacheza dhidi ya Morocco.

    Michuano ya Kombe la dunia ya mchezo wa Raga inatarajiwa kufanyika nchini Japan, kuanzia mwezi Septemba hadi mwezi Novemba mwaka 2019.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako