• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikapu, Usajili wa wachezaji: Lebron James akubali kujiunga na timu ya L.A. Lakers

    (GMT+08:00) 2018-07-02 10:52:56

    Hatimaye imefahamika kuwa mchezaji bora wa ligi ya kikapu nchini Marekani kwa msimu uliopita Lebron James, ataihama timu yake ya Cleveland Cavaliers.

    James amekubali kusaini mkataba ya miaka minne na Los Angeles Lakers kwa ada ya uhamisho wa dola za kimarekani milioni 154.

    Endapo atakaa miaka yote minne, mkataba huo unampa fursa nono Lebron, ya kulipwa dola milioni 35.65 kwa mwaka wa kwanza, milioni 37.43 mwaka wa pili, 39.21 kwa mwaka wa tatu na milioni 41 kwa mwaka wa nne.

    Timu zingine zilizokuwa zinamuwania James ni Philadelphia 76ers, Houston Rockets pamoja na Cleveland Cavaliers wenyewe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako