• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sababu za wageni kupenda kufungua mashtaka ya hakimiliki nchini China zatajwa

    (GMT+08:00) 2018-07-02 18:18:51

    Wakati wa Marekani kuanza kutoza ushuru dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya bilioni 34 unapowadia, vita kubwa zaidi ya kibiashara kati ya China na Marekani tangu zilipoanzisha uhusiano wa kibalozi, inakaribia kulipuka. Moja ya sababu za Marekani kuanzisha vita hiyo, inasema ni uzembe wa China katika ulinzi wa hakimiliki, lakini huo si ukweli.

    Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na tovuti ya Raconteur ya Uingereza, katika miaka ya hivi karibuni, China imekuwa nchi inayopendelewa na makampuni ya nje kushughulikia migogoro ya hakimiliki kutokana na kutoa hukumu kwa uwazi na haki. Mwaka 2015 mashirika 65 ya nchi za nje yalifungua mashtaka ya ukiukaji wa hakimiliki dhidi ya makampuni mengine ya nje kwenye mahakama ya hakimiliki ya Beijing, na kupata ushindi kwenye kesi zao. Makala moja iliyochapishwa mwaka huu kwenye jarida la The Diplomat la Marekani inasema, kuanzia mwaka 2006 hadi 2011, idadi ya kesi za hakimiliki zilizofunguliwa nchini China na makampuni ya nje ilichukua zaidi ya asilimia 10 ya kesi zote za aina hiyo, na asilimia 70 kati yao zilipata ushindi.

    Jaji wa mahakama ya hakimiliki katika Mahakama kuu ya China Bw. Song Xiaoming amedokeza kuwa asilimia 30 ya kesi zilizofunguliwa kwenye mahakama ya hakimiliki ya Beijing zinahusisha makampuni ya nje, na kiasi kikubwa kati ya kesi hizo, mshtaki na mshutakiwa wote ni wageni. Hali hii inaonesha kuwa wageni wanapenda kushughulikia migogoro yao kuhusu hakimiliki nchini China, haswa ile inayohusiana na vigezo na hataza.

    Mbali na sifa nzuri ya mahakama ya China ya kutoa hukumu kwa haki, muda mfupi wa kutolewa hukumu pia ni sifa nyingine nzuri. Muda wa wastani wa kushughulikia kesi za hakimiliki kwenye mahakama ya hakimiliki ya Beijing ni miezi minne hivi, ikilinganishwa na miezi 18 ya nchi za Umoja wa Ulaya, na nchini Marekani kipindi cha maandalizi ya kesi za hataza huchukua zaidi ya miezi 29.

    Makampuni mengi zaidi ya nchi za nje kuchagua kufungua mashtaka ya hakimiliki nchini China, kunaakisi kuwa yanakubali na kuwa na imani na Mfumo wa kulinda hakimiliki wa China.

    Rais Xi Jinping wa China ameagiza kuimarisha mapambano dhidi ya vitendo vya kukiuka hakimiliki, na kuwaadhibu vikali wahusika wa vitendo hivyo kwa mujibu wa sheria. Anaona kuwa kuimarisha ulinzi wa hakimiliki si kama tu ni jambo muhimu katika kukamilisha mfumo wa kulinda hakimiliki wa China, na bali pia ni kichocheo kikubwa cha kuinua nguvu ya ushindani ya uchumi wa China. Kwenye Mkutano wa mwaka huu wa Baraza la Boao, rais Xi alisema, China inahamasisha makampuni ya China na ya nchi za nje kufanya ushirikiano na mawasiliano ya kiteknolojia, na kuzingatia ulinzi wa hakimiliki halali za makampuni ya nje nchini China; wakati huohuo China pia inazitaka serikali za nchi za nje kuimarisha ulinzi wa hakimiliki za China.

    Takwimu zinaonesha kuwa kuanzia mwaka 2001 malipo ya hakimiliki yaliyotolewa na China kwa nje yameongezeka kwa asilimia 17 kila mwaka, na kufikia dola za kimarekani bilioni 28.6 mwaka 2017. Mwaka huo, China iliwasilisha maombi ya hataza elfu 51 kwa Shirika la hakimiliki duniani WIPO, idadi ambayo ilichukua nafasi ya pili duniani, baada ya Marekani.

    Wachambuzi wanaona kuwa, serikali ya Marekani kuzusha vita ya biashara dhidi ya China kwa kisingizio cha hakimiliki, kunalenga kuzuia maendeleo ya sayansi na teknolojia za China, na maendeleo ya uchumi wa China. China haitaki, lakini haiogopi vita ya biashara, na itajibu mapigo kithabiti na kwa hatua madhubuti nchi yoyote inayozusha vita hiyo. Wakati huohuo China pia itaendelea kuongeza nguvu katika kulinda hakimiliki, na kuendelea na juhudi za kuendeleza sayansi na teknolojia zake za hali ya juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako