• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuendeleza aina mpya ya roketi za kubeba mizigo

    (GMT+08:00) 2018-07-02 18:44:30

    Msanifu mkuu wa Taasisi ya utafiti wa teknolojia ya maroketi ya China, ambaye pia ni mwanachama wa Akamedia ya uhandisi ya China Bw. Long Lehao amesema, China inalenga kuendeleza mfululizo mpya wa maroketi ya Long March yatakayokuwa na uwezo wa kubeba mizigo yenye ukubwa tofauti ifikapo mwaka 2030, ili kukidhi mahitaji ya operesheni zake za anga ya juu.

    Bw. Long amesema hayo alipokuwa akihutubia katika Chuo Kikuu cha Tsinghua. Amesema uwezo wa maroketi ya China utafikia kupeleka tani 140 kwenye obiti ya chini ya kuzunguka dunia, tani 44 kwenye obiti ya kwenda sayari ya Mars, na tani 50 kwenye obiti ya kwenda Mwezi.

    China imebuni zaidi ya aina 10 za maroketi ya kubeba mizigo, kupeleka zaidi ya vyombo 400 kwenye anga za juu, ikiwemo zaidi ya satelite 60 za kibiashara zilizorushwa kwa ajili ya nchi zaidi 20.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako