• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • AIIB yaidhinisha uwekezaji wa dola bilioni 5.3 katika "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

  (GMT+08:00) 2018-07-02 19:03:28

  Mkuu wa Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia AIIB Bw. Jin Liqun amesema, benki hiyo inaunga mkono pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" lililotolewa na China, na imeidhinisha uwekezaji wa dola za kimarekani bilioni 5.3 katika miradi inayohusika kwenye nchi za sehemu zilizoko "Ukanda mmoja Njia moja" katika miaka miwili na nusu iliyopita.

  Bw. Jin amesema hayo kwenye mkutano wa baraza la kimataifa la ushirikiano wa kisheria la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" uliofanyika mjini Beijing.

  Amesisitiza kuwa, utekelezaji wa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" limepata maendeleo makubwa, na mkutano huo utasaidia pande zote husika kufahamu pendekezo hilo kwa usahihi na ukamilifu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako