• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • LIANG JIA HE 3

    (GMT+08:00) 2018-07-02 19:44:06


    Baada ya kufika katika Kijiji cha Liang Jiahe, kijana Xi Jinping alifanya kazi kama mkulima, huku akijitahidi kusoma vitabu vingi ili kupata virutubisho kutokana na vitabu ambavyo vinaweza kujenga vizuri roho na fikra zake.
    Wanakijiji wa Liang Jia He wamepata kumbukumbu moja, kwamba Xi Jinping alipokuwa kijijini alisoma sana vitabu, alipokuwa anakula alisoma, alipokuwa anachunga kondoo mlimani pia alisoma.
    Wakati ule kijijini hakukuwa na umeme, muda mfupi baada ya giza kuingia, kijijini kote watu wengi walilala mapema. Isipokuwa kwenye nyumba ya pango la mlima ya Xi Jinping, ilikuwa bado ina mwanga uliofifia wa taa ya mafuta, hakuna mtu aliyejua, mwanga huu wa taa ulimpa mwanga mkubwa wa namna gani moyoni mwake. Vijana wasomi wa Beijing waliofanya kazi katika wilaya ya Yanchuan walikuwa wanasoma katika sekondari zaidi ya kumi mjini Beijing, wote walikwenda kijijini na vitabu vyao, na kila mara walibadilishana vitabu na kusoma sana vitabu vyote.

    Xi Jinping pia alisoma vitabu vingi vya Urusi. Alipokumbuka alisema: "Watu wa kizazi chetu tulipata ushawishi mwingi kutoka kwenye vitabu maarufu vya Urusi, kutokana na vitabu hivyo vilivyoandikwa na waandishi maarufu wa vitabu wa Urusi nilijifunza mengi sana, kuelewa watu wa namna gani ni mashujaa, mabadiliko makubwa ya zama kubwa na mawazo, hisia na mienendo ya watu, hata tuliweza kujitakasa kiroho na kujijenga.".

    Baada ya kuishi kijijini Liang Jia He kwa miaka miwili mitatu hivi, Xi Jinping alijua kuongea vizuri kwa maneno wanayotumia wenyeji wa Yanchuan, hata baada ya kuondoka huko anajua pia kuongea maneno ya wenyeji wa huko.

    Alipofanya kazi kijijini, kulima mashamba, kubeba samadi, kupanda mimea, kupalilia, kuvuna na kubeba nafaka, kila kazi alifanya kama wengine walivyofanya. Xi Jinping alijifunza kwa makini kutoka kwa wanakijiji, akikutana na taabu aliwauliza na kufundishwa nao, siku hadi siku, akazoea kazi zote na kuwa mkulima mwenye uwezo wa kweli.

    Mbali na kazi mbalimbali za mashambani, Xi Jinping alijifunza kufanya kazi za kusokota nyuzi za sufu, kushona viraka kwenye nguo, kuandaa matandiko kitandani, kila kitu alifanya mwenyewe. Alisema, amekuwa na uwezo mkubwa kushughulikia kila kitu cha maishani, aliwekewa msingi wakati alipofanya kazi na kuishi kijijini. Xi Jinping alisema: "Muhimu zaidi, nimejifunza moyo wa wakulima wa kutafuta ukweli kwa kufuata hali halisi, kufanya kazi bila kuogopa taabu na kuwa na uvumilivu mbele ya changamoto, mimi ni mkulima."

    Katika Kijiji cha Liang Jia He, kulikuwa na mtu mmoja ambaye alikuwa hapendi kufanya kazi za sulubu, kila mara alirandaranda hata aliiba vitu, hivyo aliwekwa kwenye orodha ya "watu wanaosimamiwa", lakini yeye mwenyewe hakukubali kusimamiwa. Wanakijiji kila mara waliitisha mkutano kumkosoa hata kumtukana, lakini Xi Jinping hakumtukana, bali alimkosoa kwa upole na kumtaka ajisahihishe. Huyu mkorofi alimsikiliza na kukubali. Baadaye Xi Jinping na Lei Pingsheng walimtaka aimbe wimbo mmoja wa kienyeji, mara hali wasiwasi kwenye mkutano ikaondolewa.

    Baadaye mtu huyo alisema, mimi nitajifunza kutoka kwa watoto kutoka Beijing, sitathubutu tena kuiba. Xi Jinping alitumia njia hii iliyojaa hisia za upendo kumfundisha mtu aliyefanya makosa, akasifiwa sana na wanakijiji wa Liang Jia He, wote walisema: "Kweli watoto kutoka Beijing wana uwezo".  Na baadaye mtu huyu akajirekebisha na kushiriki kwenye kazi za sulubu. Xi Jinping alisema: "Huyu mtu alifanya makosa madogo tu aliweza kujisahihisha, tunatakiwa kumfundisha tu badala ya kumtukana".

    Mzee Liang Yuming alisema, Xi Jinping aliwaheshimu watu, kuwasaidia na kushikamana nao, kweli anajua mengi zaidi. Siku hadi siku, eneo alipokaa Xi Jinping limekuwa kiini cha Kijiji cha Liang Jia He, watu wengi walipenda kumtembelea, kupiga soga naye, kusikiliza akielezea historia, na habari mpya nje ya kijiji, kweli alikuwa mmoja wa wanakijiji wa Liang Jia He.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako