liangjiahe4.
|
Mwezi Januari mwaka 1974, wakati majira ya baridi kali yamewadia kwenye Uwanda wa Juu wa Udongo Manjano, na kukaribia Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, wanakijiji wa Liang Jia He walianza kuwa na pilikapilika za maandalizi ya kununua vitu kwa ajili ya sikukuuu.
Wakati huo ilikuwa ni muda mfupi baada ya Xi Jinping kuchaguliwa kuwa katibu wa tawi la Chama la Kikosi cha tarafa cha uzalishaji, na siku zote alifikiri jinsi ya kufanya mambo halisi kwa ajili ya kubadilisha sura ya Liang Jia He, na kuhimiza maendeleo yake.
Siku moja Xi Jinping alipokuwa anasoma gazeti, aliona maelezo kuhusu mkoa wa Sichuan kutoa nguvu kubwa katika ujenzi wa mashimo ya gesi za kinyesi, alivutiwa sana habari hiyo. Alifikiria kama kijiji aliko kitaweza kutumia gesi ya kinyesi kupika chakula na kuwasha taa, itawanufaisha sana wanakijiji.
Liang Jia He ni kijiji cha mbali, wanakijiji wakitaka kupata makaa ya mawe walilazimika kwenda kwenye mgodi ulioko mbali kuyachukua. Hivyo kwa muda mrefu watu wa huko walikata miti ili kupata kuni za kupikia, hali hii ilisababisha mmomonyoko wa ardhi, na kuahtiri maendeleo ya kilimo. Kama watajenga mashimo ya gesi ya kinyesi, si kama tu wataweza kuondoa tatizo la nishati kijijini, kukomboa nguvukazi, bali pia wataweza kushughulikia kinyesi, kuinua kiwango cha usafi wa umma kijijini, kutatua tatizo la mbolea kijijini, na kuongeza utoaji wa nafaka. Gesi ya kinyesi ni ufunguo wa matatizo kwenye uzalishaji wa kilimo na maisha ya wanakijiji.
Gesi ya kinyesi ilikuwa ni jambo jipya kabisa wakati ule, ingawa Xi Jinping alikuwa na matarajio mazuri, lakini alifikiri kwa makini sana, aliona hali ya hewa ya mkoa wa Sichuan na sehemu ya Shanbei ni tofauti sana, wakiiga uzoefu wao watafaulu au la?
Xi Jinping siku zote na mtendaji mwenye juhudi. Yeye na wenzake wawili walikwenda mkoa wa Sichuan kufahamishwa ipasavyo jinsi walivyofanya ujenzi wa mashimo ya gesi ya kinyesi, na kujifunza kutoka kwao.
Baada ya kurudi Liang Jia He, Xi Jinping aliimarisha nia ya kujenga mashimo ya gesi ya kinyesi, akaanza kueleza manufaa ya gesi hiyo, na kuwakusanya vijana wa kijijini kufanya majaribio. Lakini matatizo magumu waliyokutana nayo ni magumu sana, tofauti na walivyodhani awali.
Suala la kwanza kujenga shimo la majaribio la gesi ya kinyesi kwenye sehemu gani kijijini. Halafu namna ya kusafirisha raslimali za ujenzi, baada ya kukamilisha ujenzi, watasafirisha gesi kwa namna gani. Kazi ngumu zaidi ni kuwa, Liang Jia He hakuna mawe yaliyofaa kutengenezwa kuwa vipande vya mawe vya kuwa kifuniko wa shimo.
Xi Jinping na wenzake walitatua tatizo moja baada ya lingine, waliona kufanya juhudi ndiyo kupata ufumbuzi. Baada ya kufanya upimaji mara kwa mara, mwishowe walijenga shimo la majaribio kwenye eneo karibu na makazi ya vijana wasomi, kijiji chao hakikuwa na mawe, Xi Jinping aliwaongoza vijana kuchimba udongo kwa kina wakayapata; hakukuwa na mchanga, Xi Jinping aliwaongoza vijana kwenda sehemu ya mbali kuchimba na kuubeba kurudi kijijini kila siku mara mbili, na hakuna mtu hata mmoja aliyelalamika kwa sababu ya taabu na uchovu, vilevile Xi Jinping alikwenda kujifunza kutoka kwa fundi halafu wakajenga uwanja mdogo wa kuchoma chokaa...Kila mtu alikuwa na nia imara ya kufaulu kujenga shimo la gesi ya kinyesi, na wote hao walikuwa na pilikapilika bila kusita. Hata hivyo kulikuwa na watu waliotia mashaka juu ya kazi yao, walidhani vijana hao watashindwa kufanya kazi hii. Na baadhi walisema gesi ya kinyesi haiwezi kutumiwa kupika chakula na kuwasha taa za nyumbani.
Lakini Xi Jinping alishikilia nia yake imara aliamini watafanikiwa na hatimaye kuwaonesha hali halisi.
Katikati ya mwezi Julai mwaka 1974, shimo lenye ujazo wa mita nane hivi la gesi ya kinyesi lilikamilika, lakini mwanzoni haliwekuza kutoa gesi. Xi Jinping alichunguzachunguza na kuondoa tatizo, na hatimaye lilianza kutoa gesi!
Habari hii ya mafanikio ilienea haraka kote kijijini, na hata katika maeneo mengine na wilayani, watu wakamiminikia Liang Jia He kuangalia nishati ya moto wa gesi ya kinyesi.
Xi Jinping na wenzake walijenga shimo la kwanza la gesi ya kinyesi la mkoa wa Shanxi wakati ule, wanakijiji walishuhudia ufanisi wa matumizi ya gesi ya kinyesi kwa kuwasha taa na kupika chakula, wakaongeza ari ya kuendelea kujenga mashimo ya gesi ya kinyesi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |