• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makamu wa Rais wa China akutana na mwenyekiti wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2018-07-02 20:45:43

    Makamu wa rais wa China Bw. Wang Qishan leo hapa Beijing amekutana na mwenyekiti wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Bw. Miroslav Lajcak.

    Bw. Wang Qishan amesema, China inapenda kutimiza maendeleo kwa pamoja na nchi mbalimbali chini ya mfumo wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kuendelea kuunga mkono utaratibu wa pande nyingi, na kuunga mkono Umoja wa Mataifa kuchukua nafasi ya uongozi kwenye jumuiya ya kimataifa, na kuchangia busara na nguvu ya China katika kujenga utaratibu wenye usawa na haki wa usimamizi wa dunia.

    Bw. Lajcak amesema, China ikiwa ni mwungaji mkono mkubwa wa utaratibu wa pande nyingi, na mhimizaji muhimu wa amani na maendeleo ya dunia, Umoja wa Mataifa unapenda kukuza ushirikiano wa pande nyingi kati yake na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako