Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje wa China Bw. Lu Kang amesema China itaendelea kuunga mkono kupunguza taharuki kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini, na pia inatumai kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.
Bw. Lu Kang amesema China inafurahia Korea Kaskazini na Korea Kusini kuongeza mawasiliano, na kufikia makubaliano mbalimbali. Pia inatumai kuwa jumuiya ya kimataifa itaweka mazingira mazuri kwa ajili ya kuimarisha mwelekeo huo, kuhimiza mchakato wa kuondoa silaha za nyuklia kwenye Peninsula ya Korea, na kusukuma mbele ufumbuzi wa kisiasa wa suala la Peninsula ya Korea.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |