• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzia, Masumbwi Uganda: Bondia Katende afariki akifanya mazoezi

    (GMT+08:00) 2018-07-03 10:57:09

    Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini Uganda Mustafa Katende ameanguka gafla na kufariki dunia wakati akiwa mazoezini jana asubuhi mjini Kampala.

    Kwa mujibu wa msimamizi mkuu wa kituo cha mazoezi cha polisi kibuli cha mjini Kampala Afande Dan Kasole, bondia Katende alikuwa anasita kufanya mazoezi jana kwa kujihisi kuwa hayuko fiti.

    Lakini Muda mfupi baada ya mwalimu wa bondia huyo kufika, walikubaliana afanye awamu mbili za mazoezi mepesi, lakini jambo hilo ndilo lililomchosha na kumfanya apoteze nguvu na kisha kuanguka, na licha ya jitihada za haraka za kumpa huduma ya kwanza na kumkimbiza hospitali kufanyika, hazikuokoa maisha yake.

    Madaktari wa Hospitali ya Nsambya ambayo iko karibu na kituo hicho cha mazoezi walisema sababu za kifo cha Katende ni shambulio la moyo.

    Bondia alikuwa akifanya mazoezi kwa ajili ya pambano lake lililokuwa lifanyike Julai 30 mwaka huu nchini Poland.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako