• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikapu: Wachezaji 9 wa Ufilipino, 4 wa Australia watolewa uwanjani kutokana na vurugu

    (GMT+08:00) 2018-07-03 11:03:11

    Timu ya taifa ya Ufilipino ya mchezo wa mpira wa kikapu jana ililazimika kumalizia mchezo wake dhidi Australia ikiwa na wachezaji watatu uwanjani kutokana na vurugu zilizotokea kwenye mechi yao ya kufuzu kombe la dunia iliyofanyika mjini Manila.

    Jumla ya wachezaji 9 wa timu hiyo walitolewa kutokana na utovu wa nidhamu ikiwemo kupigana, na kurushiana viti.

    Licha ya timu ya Australia kupata ushindi wa alama 89-53, wachezaji wake wanne waliondolewa pia.

    Kutokana na vurugu hizo, shirikisho la mpira wa kikapu duniani FIBA, limetangaza kuwa litachunguza na kuchukua hatua kutokana na tukio hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako