• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la dunia: Brazil na Ubelgiji zafuzu robo fainali

    (GMT+08:00) 2018-07-03 11:04:35

    Timu za taifa za Brazil na Ubeligiji zimefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia inayoendelea nchini Urusi baada ya kupata ushindi kwenye mechi za hatua ya 16 bora zilizopigwa jana.

    Brazil ilipata ushindi wa magoli mawili 2-0 dhidi ya Mexico yaliyofungwa Neymar Dos Santos pamoja na Roberto Firmino.

    Nao Ubeligiji, licha ya kutangulia kufungwa magoli 2-0 na Japan, walifanikiwa kusawazisha, na baadaye wakapata ushindi wa magoli 3-2.

    Kutokana ushindi huo, timu hizo mbili sasa zitakutana kwenye hatua ya robo fainali siku ya ijumaa Julai 6.

    Michuano hiyo inaendelea kwa mechi mbili, ambapo Sweden watacheza na Uswisi na Uingereza watacheza na Colombia

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako