• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ataka mbinu bora zienezwe ili kusukuma mbele maendeleo ya kazi mbalimbali

    (GMT+08:00) 2018-07-03 18:10:25

    Rais Xi Jinping wa China ameupongeza mji wa Qingdao kutokana na maandalizi mazuri ya Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai SCO, na kutaka mbinu bora zienezwe na maadili bora yaenziwe, ili kusukuma mbele maendeleo ya kazi mbalimbali.

    Rais Xi amesisitiza kuwa kuandaa mkutano huo kumetoa fursa mpya kwa mji wa Qingdao na mkoa wa Shandong, na amezitaka serikali za miji na mikoa mbalimbali zijifunze uzoefu huo, na kueneza mbinu bora na maadili bora yaliyoakisiwa kwenye maandalizi ya mkutano huo.

    Mkutano wa kilele wa 18 wa SCO ulifanyika kwa mafanikio mjini Qingdao mkoani Shandong kuanzia tarehe 9 hadi 10 mwezi Juni. Huu ni mkutano mkubwa zaidi, wa ngazi ya juu zaidi na wenye matunda mengi zaidi wa SCO kufanyika tangu jumuiya hiyo ilipoanzishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako