• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kurekebisha muundo wa uchukuzi ili kupunguza uchafuzi wa hewa

    (GMT+08:00) 2018-07-03 18:23:28

    Naibu waziri wa uchukuzi wa China Bw. Liu Xiaoming amesema, katika miaka mitatu ijayo, China itarekebisha muundo uliopo wa uchukuzi wa mizigo unaotegemea zaidi barabara, na kuhimiza usafirishaji wa mizigo kwa njia za reli na meli, ili kuunga mkono juhudi za kupunguza uchafuzi wa hewa.

    Bw. Liu Xiaoming pia amesema, ili kutimiza lengo hilo, mbali na kuongeza ufanisi wa uchukuzi wa reli, China itachukua hatua mbalimbali kuboresha mfumo wa uchukuzi wa majini, kuanzisha kampeni ya kusimamia uchukuzi wa barabara, kuunganisha njia mbalimbali za uchukuzi, na kujenga eneo la kielelezo cha marekebisho ya muundo wa uchukuzi kwenye miji ya Beijing, Tianjin na mkoa wa Hebei pamoja na sehemu za karibu, ili kuboresha muundo wa uchukuzi kote nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako