• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • LIANG JIA HE 6

    (GMT+08:00) 2018-07-03 21:02:33

    Sera ya kufanya mageuzi na kufungua mlango imewawezesha wakulima wa Liang Jiahe waishi maisha mazuri.

    Liu Ruilian alikuwa mtoto wa familia maskini. Anakumbuka kuwa, alipokuwa mtoto, yeye na wadogo wake hakuwahi kuvaa viatu wakati wa siku za joto, na wakati wa usiku kweye kitanda cha udongo, yeye na wadogo wake yaani watoto wane walikuwa na dandiko moja tu, wakati ule hata walikuwa hawathubutu kutamani kupata chakula cha unga wa ngano.

    Alipokuwa na umri wa miaka 17, Liu Ruilian aliolewa na mwanakijiji Gong Zhengfu wa kijiji chao Liang Jia He. Baada ya kuolewa, maisha ya familia yake bado ni magumu sana, hawakuweza kupata chakula cha kutosha, kila mara waliweza kula mboga wa aina mbalimbali mwituni, hata baada ya kula kila mara walipata uvimbe mikononi na nyusoni.

    Xi Jinping alipokuwa katibu wa tawi la Chama la Liang Jia He, aliwashirikisha wanakijiji kuanzisha ushirika wa vyombo vya kilimo, duka la kuuza vitu vya lazima maishani, na ushirikiano wa ushonaji nguo. Liu Ruilian alichaguliwa kuwa mshonaji mmoja, alifurahi sana hata alishindwa kupata usingizi kwa usiku mmoja.

    Baada ya kuwa mshonaji wa nguo Liu Ruilian alichapa kazi sana, hata alikopa pesa kununua cherahani na kushona nguo nyumbani kwa ajili ya ushirika wake.

    Familia ya Liu Ruilian wameanza kuishi maisha mazuri kama wakulima wengine wa eneo la Shaanbei, kila ifikapo majira ya mavuno, Liu Ruilian alifurahi sana akiangalia nafaka zilizovunwa zikijaa kwenye nyumba yao ya pango.

    Na baadaye kila akipata nafasi alikwenda mjini kufanya kazi za kibarua, Liu Ruilian hajakuwa na wasiwasi tena kuhusu chakula na matumizi ya familia yake, kwa mara ya kwanza ameanza kujiridhika na maisha yake.
    Kufanya mageuzi kumeleta mabadiliko ambayo yasiyotokea hapo kabla katika Kijiji cha Liang Jia He; na kufungulia mlango kumeleta uwezekano usio na uomo kwa mabadiliko hayo.

    Mwaka 1993, Xi Jinping aliyekuwa katibu wa Kamati ya Chama ya Fuzhou alirudi Liang Jia He, alipoona wanakijiji hawana wasiwasi tena juu ya chakula na nguo, alifurahi sana kama wanakijiji wallivyo, kwani kupata chakula na nguo za kutosha kulikuwa matarajio yake na wanakijiji wote wakati ule, sasa ameona kila familia ina chakula za kutosha hakika anafurahi kweli kutoka moyoni.

    Tarehe 18 Oktoba, 2017, wanakijiji wa Liang Jia He walikusanyika kwenye ofisi ya tawi la Chama la kijiji, wakitazama televisheni pamoja na kutaka kuangalia ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China.
    Wakati huo kwenye Ukumbi mkubwa wa Jumba la mikutano ya umma la Beijing washiriki walipiga makofi ya furaha bila kusita, hali kadhalika katika ofisi hiyo ya Liang Jia He. Waliposikiliza ripoti aliyotoa Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chana Xi Jinping, wanakijiji waliona maneno yote yanagusu miyoyo yao.

    Wanakijiji walijadili kwa furaha na wakaongeza imani ya kujenga siku zao nzuri zaidi za baadaye.

    Liang Jia He, kijiji kimoja kidogo cha kawaida mlimani, zamani watu wa kijiji hiki walikuwa na matarajio, hivi sasa wanafanya matarajio mengi kuwa hali halisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako