• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • EAC: Wanawake wa Afrika mashariki waongeza soko ulaya

    (GMT+08:00) 2018-07-03 20:27:34

    Wanawake wafanya biashara wa Afrika mashariki kupitia kwa jukwaa lao wamefanikiwa kujadili makubaliano na Kituo cha Kimataifa cha Biashara (ITC) ili kuongeza soko la bidhaa zao Ulaya.

    Mkurungezi mkuu wa kituo hicho Arancha Gonzalez, ameyasema hayo wakati akiwa kwenye mkutano na wanawake hao katika makao makuu ya jumuiya ya Afrika mashariki mjini Arusha.

    Naye mkurungezi wa baraza la kibiashara la Afrika Mashariki, Lilian Awinja amesema wamefanya utafiti kuhusu bidhaa wanazoweza kuuza kwa wingi ikiwemo kahawa, maua, samaki chai mboga na matunda.

    Kulingana na kituo cha kimataifa cha biashara kanda ya Afrika Mashariki imeuza bidhaa za dola 2.5 mwaka 2017 likiwa ni ongezeko la asilimia 8 kutoka mwaka 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako