• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kriketi Wanawake, Kufuzu Mashindano ya Dunia: Uganda kuanza mechi zake Julai 7

    (GMT+08:00) 2018-07-04 10:22:41

    Timu ya taifa ya Uganda ya Cricket Wanawake (Lady Cricket Cranes) imeagwa rasmi kwa ajili ya kwenda uholanzi kushiriki mechi za kufuzu mashindano ya dunia zinazotarajiwa kuanza julai 7 na kumalizika julai 14 mwaka huu.

    Uganda ilipata nafasi ya kwenda kushiriki michuano ya kufuzu baada ya kuzifunga timu za Tanzania na Zimbabwe kwenye mechi za awali mwezi Mei mwaka huu.

    Kwenye michuano hiyo ya kufuzu Uganda itacheza mechi tatu, moja dhidi ya Scotland, nyingine na Thailand na dhidi ya Ireland, na itakuwa ni tarehe 7, 8 na 10 mtawalia, lakini kabla ya hapo inatarajiwa pia kucheza mechi ya kirafiki ya maandalizi dhidi ya timu ya Umoja wa Falme za Kiarabu kesho mei 5.

    Katika viwango vya ubora barani Afrika, timu hiyo ya Uganda kwa sasa inashika nafasi ya pili nyuma ya Afrika Kusini, na duniani inashika nafasi ya 18.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako