• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raga: Timu ya Zimbabwe yalala nje kufuatia hadhi mbaya ya hoteli nchini Tunisia

    (GMT+08:00) 2018-07-04 10:23:04

    Katika hali isiyokuwa ya kawaida, timu ya taifa ya Zimbabwe ya mchezo wa raga ambayo inatarajiwa kucheza mechi ya kufuzu kombe la Dunia siku ya jumamosi dhidi ya Tunisia jana imeushtua ulimwengu baada ya wachezaji wake kuamua kulala nje kando ya barabara ya mtaa baada ya kutokubaliana na hadhi ya hoteli iliyoandaliwa kwa ajili yao.

    Wachezaji hao walionekana kwenye mtaa mmoja wakiwa wamelala huku wamejifunika mablanketi binafsi waliyokuja nayo, na wakionekana kuwa pamoja na masanduku yao ya kusafiria, na mizigo mingine ya timu.

    Kufuatia hilo na taharuki iliyoibuka, chama cha Raga cha Tunisia kimeiomba radhi timu hiyo, na kusema kwamba hoteli waliyopangiwa haikuwa sehemu ya mpango wa ushindi kama ambavyo imetafsiriwa na mashabiki wa michezo.

    Aidha chama cha raga cha Afrika pia kimeomba radhi kwa Zimbabwe kutokana na sakata hilo na kwamba uchunguzi unaendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako