• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Kagame Cup-Tanzania: Gor Mahia yapata sare kwa mara nyingine tena

    (GMT+08:00) 2018-07-04 10:23:27

    Gor Mahia ya Kenya ikicheza mchezo wa pili jana imelazimishwa sare ya mabao 2-2 na timu ya Lydia Ludic ya Burundi.

    Magoli yote ya Gor yalikuwa ni ya kusawazisha baada ya Ludic kutangulia kufunga mara mbili, yakifungwa Philemon Otieno pamoja na Jacques Tuyisenge katika dakika ya 90 kwa njia ya penati.

    Katika mechi nyingine ya kundi hilo iliyopigwa jana, Rayon Sports ya Rwanda, pia imetoka sare ya bao 1-1 na AS Ports ya Djibouti.

    Matokeo hayo yote yameifanya Ports kukaa kileleni mwa Kundi B ikiwa na pointi nne ikifuatiwa na Gor Mahia halafu Rayon ambazo zote zina pointi mbili kila moja lakini Lydia yenyewe ipo mkiani ikiwa na pointi moja tu.

    Michuano hiyo inaendelea leo, ambapo Vipers ya Uganda itacheza na Kator FC ya Sudan Kusini, Azam FC itavaana na JKU ya Zanzibar, APR itacheza dhidi ya Dakadaha ya Somalia na Simba ya Tanzania itacheza dhidi ya Singida United ya Tanzania pia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako