• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la Dunia 2018: Sweden yafuzu robo fainali baada ya miaka 24

    (GMT+08:00) 2018-07-04 10:23:53

    Timu ya taifa ya Sweden jana imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia baada ya kuifunga Uswisi kwa goli 1-0 katika mechi ya hatua ya 16 bora.

    Goli pekee la Sweden lilifungwa na Emil Forsberg, na kuifanya timu hiyo ifuzu hatua hiyo kwa mara nyingine baada ya miaka 24 kupita tangu ifanye hivyo mara ya mwisho mwaka 1994 kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Marekani.

    Kwa kufuzu hatua ya robo fainali, siku ya jumamosi Julai 7, Sweden sasa itacheza na Uingereza ambayo pia imefuzu jana baada ya kuishinda Colombia kwa njia ya penati katika mechi ya hatua ya 16 bora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako