• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa saba wa jumuiya za washauri bingwa za China na Afrika wafunguliwa mjiini Beijing

    (GMT+08:00) 2018-07-04 10:24:40

    Mkutano wa saba wa jumuiya za washauri bingwa za China na Afrika umefunguliwa leo asubuhi mjini Beijing.

    Kwenye ufunguzi wa mkutano huo msaidizi wa waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Chen Xiaodong, amesema katika kipindi cha miaka 40 tangu China ilipoanza kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, ushirikiano kati ya China na Afrika umepata maendeleo makubwa, na kuwa na manufaa kwa watu wa pande mbili. Amesema licha ya ukosoaji kutoka baadhi ya nchi za magharibi, uhusiano kati ya pande mbili umeendelea kustawi.

    Mkutano huo wa siku mbili, ni moja ya shughuli za maandalizi ya mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika unaotarajiwa kufanyika mwezi septemba hapa Beijing. Wajumbe 380 ikiwa ni pamoja na maofisa wa balozi 44 za nchi za Afrika, maofisa wa serikali, wanataaluma kutoka taasisi za washauri bingwa kutoka pande mbili wanashiriki kwenye mkutano huo.

    Ajenda kuu ya mkutano huo ni "maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika katika miaka 40 ya sera ya mageuzi na ufunguaji mlango ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako