• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yapinga kauli ya nchi za magharibi kwamba "utoaji wa mikopo wa China umeongeza mzigo wa madeni ya Afrika"

  (GMT+08:00) 2018-07-04 18:12:30

  Msaidizi wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Chen Xiaodong leo amekanusha kauli ya nchi za magharibi kuwa utoaji wa mikopo wa China umeongeza mzigo wa madeni kwa nchi za Afrika, akieleza kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika umepata mafanikio makubwa, na kuwanufaisha watu wa pande zote mbili.

  Akihutubia sherehe ya ufunguzi wa mkutano wa 7 wa Baraza la washauri bingwa wa China na Afrika Bw. Chen Xiaodong anasema:

  "Tukitupia macho miaka kadhaa iliyopita, uhusiano na ushirikiano kati ya China na Afrika umepata mafanikio makubwa na kuwanufaisha wananchi wa pande zote mbili. Lakini baadhi ya watu wa nchi za Magharibi hawapendi kuacha upuuzi wala hawataki kuona ushirikiano kati ya China na Afrika ukipata maendeleo, badala yake wanatoa kauli za kupotosha kuhusu ushirikiano wa pande hizi mbili, na kulaani utoaji wa mikopo wa China kwamba umeongeza mzigo wa madeni ya China, na China inaingilia kati mamlaka ya nchi za Afrika kwa njia ya kutoa fedha, hali ambayo imeonesha moyo wao wenye wivu."

  Bw. Chen Xiaodong amesisitiza kuwa, ushirikiano kati ya China na Afrika siku zote unaheshimu nia na mahitaji ya nchi za Afrika, kushikilia kufanya mashauriano kwa usawa bila ya kuweka sharti lolote la siasa, hali ambayo inatofautiana kabisa na nchi za magharibi, na inakubaliwa na kukaribishwa na nchi za Afrika.

  Bw. Chen Xiaodong anaona kuwa, suala la madeni ya Afrika linatokana na sababu nyingi, na linalikabili nchi nyingi zinazoendelea. Bw. Chen anasema:

  "Utatuzi wa suala la madeni ya Afrika unapaswa kutegemea maendeleo. China imekuwa ikiratibu mipango ya maendeleo ya China na nchi za Afrika, ili kuzisaidia nchi hizo kuongeza uwezo wa kujiendeleza, na kuanzisha miradi mingi inayonufaisha maisha ya wananchi barani Afrika."

  Bw. Chen Xiaodong pia ameeleza kuwa, huu ni mwaka muhimu kwa uhusiano kati ya China na Afrika, na mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika mwezi Septemba unafuatiliwa na dunia. China na Afrika zitatumia fursa hii nzuri, kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika kwa kufuata msingi wa kufanya ushirikiano wa kunufaishana, kutafuta kwa pamoja njia za maendeleo katika siku za baadaye, ili kupata maendeleo mapya katika uhusiano na ushirikiano kwa pande hizi mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako