• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yaweka mitambo ya kufuatilia mapato ya makampuni ya mawasiliano

    (GMT+08:00) 2018-07-04 20:09:42

    Tume ya Mawasiliano nchini Uganda imesema kuwa imeshanunua vifaa vipya kwa kufuatilia mapato ya kila siku ya makampuni ya simu.

    Tume hiyo imesema kuwa mfumo huo mpya unafuatilia mapato ya kila siku ya makampuni ya mawasiliano.

    Ijapokuwa mfumo huo ulitarajiwa kufuatilia tu sauti na intanenti ,UCC imesema kuwa sasa inafuatailia miamala yote ya makampuni ya mawasiliano ikiwa ni pamoja na utumaji pesa kwa njia ya simu pamoja na ushuru wa mitandao ya kijamii.

    Kwa muda sasa makampuni ya MTN na Airtel yamekuwa yakipinga matumizi ya mfumo huo mpya,zikisema kuwa mfumo huo unaingilia biashara zao za utyumaji fedha kwa njia ya simu.

    Mkurugenzi Mtendaji wa UCC Bw Godfrey Mutabazi, alisema kwa muda sasa makampuni ya mawasiliano yamekuwa yakisema mapato ya kiwango cha chini tofauti na wanayoingiza.

    Alisema sasa wana ufumbuzi wa tatizo hilo,na unafanya kazi,kwa sababu wanajua kiwango wanachoingiza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako