• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kombe la Kagame: Simba na Singida United zatinga robo fainali

  (GMT+08:00) 2018-07-05 09:21:10

  Dakika 90 zimemalizika kutoka uwanja wa Taifa kwa mechi baina ya Simba Sports Club dhidi ya Singida United kumalizika kwa matokeo ya 1-1 kwenye mchezo wa michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) huku Simba ikimaliza na kuwa kinara wa kundi C

  Kwa sare hiyo, Simba imemaliza na pointi saba, sawa na Singida United, lakini Wekundu wa Msimbazi wanaidadi kubwa ya mabao.

  Mechi nyingine za michuano hiyo, APR ya Rwanda imeichapa mabao 4-1 Dakadaha ya Somalia na kumaliza nafasi ya tatu kwenye Kundi C kwa pointi zake tatu.

  Nayo Azam fc ya Tanzania wamepata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya JKU yas Zanzibar, huku Vipers ya Uganda imeifunga Kator fc ya Sudan Kusini mabao 3-0. Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi kati ya ASPorts ya Djibouti itakutana na Gor Mahia ya Kenya, nayo Lydia Ludic ya Burundi itavaana na Rayon Sports ya Rwanda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako