• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa saba wa Baraza la washauri bingwa wa China na Afrika wafanyika Beijing

  (GMT+08:00) 2018-07-05 17:22:58

  Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika utafanyika mwezi Septemba hapa Beijing. Ukiwa sehemu moja ya maandalizi ya mkutano huo wa kilele, Mkutano wa saba wa Baraza la washauri bingwa wa China na Afrika umefanyika Beijing, ambapo umewashirikisha watu 300 wakiwemo wataalamu wa pande hizo mbili na maofisa wa serikali, na kujadili kuhusu jinsi nchi za Afrika zinavyojifunza kutokana na uzoefu wa maendeleo uliopatikana katika hatua ya ufunguaji mlango na mageuzi nchini China, na namna ya kuimarisha ushirkiano katika kipindi kijacho.

  Katika miaka mingi iliyopita, China na Afrika zimekuwa zikiboresha uhusiano kati yao hatua kwa hatua. Katika Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka 2015 mjini Johannesburg, pande hizo mbili zilithibitisha uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa kimkakati wa pande zote. Hivi sasa China imedumisha hadhi yake ikiwa mwenzi muhimu zaidi wa biashara barani Afrika kwa miaka mingi mfululizo. Kwa mujibu wa takwimu za serikali ya China, thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili imezidi dola za kimarekani bilioni 170.

  Mkuu wa Taasisi ya sera za nchi za Afrika ya Kenya Bw. Peter Kagwanja ambaye amehudhuria mkutano huo anasema:

  "Mambo muhimu ni kwamba, 'ndoto ya China' na 'ndoto ya Afrika' zimeunganishwa kwenye pendekezo la 'Ukanda mmoja, Njia moja' lililotolewa na rais Xi Jinping wa China. Pendekezo hilo si kama tu linahusisha ujenzi wa miundo mbinu, bali pia linaelekeza njia ya kufanya uvumbuzi, ambayo imeiwezesha Afrika kupata fursa ya kupata ustawi kwa amani na kuwa nguvu muhimu katika muundo wa dunia mpya. Katika mwaka 2017, China ilitoa asilimia 15.5 ya fedha kwa ajili ya miradi ya ujenzi barani Afrika, na karibu nusu ya miradi katika nchi za Afrika Mashariki inawekezwa na China."

  Profesa wa Chuo Kikuu cha Johannesburg cha Afrika Kusini Bw. Merthold Monyae anaona kuwa, baada ya miaka 40 tangu China itekeleze sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, imepata uzoefu mwingi wa kuigwa na nchi za Afrika. Anasema:

  "Uchumi wa Afrika hauwezi kupata maendeleo endelevu kwa kutegemea tu kuuza malighafi. Tuna maliasili nyingi, lakini tunatumaini kuzitengeneza kuwa bidhaa barani Afrika. Hivyo tuna matumaini kuwa China itatoa msaada mwingi zaidi kwetu, na kuanzisha kampuni nyingi zaidi za kiubia kati ya pande hizi mbili ili kuhimiza mchakato wa kuanzisha utandawazi wa viwanda barani Afrika."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako