• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya biashara ya China yasema uonevu wa kibiashara wa Marekani unaenda kinyume na wakati

    (GMT+08:00) 2018-07-05 17:32:34

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, uonevu wa kibiashara unaofanywa na Marekani kupitia kutishia kuongeza ushuru unaenda kinyume na wakati, na kuongeza kuwa, kama Marekani itatekeleza hatua ya kuongeza ushuru, China itapaswa kulipiza kisasi ili kulinda maslahi ya nchi na ya umma.

    Ripoti zinasema, hivi karibuni Marekani imetishia tena kuongeza ushuru kwa bidhaa zote zinazotoka China zenye thamani ya dola bilioni 500 za kimarekani. Mbali na China, Marekani pia imetoa tishio kwa wenzi wengine wa biashara.

    Bw. Gao amesema, China haitarudi nyuma ikikabiliwa na tishio, na haitabadilisha nia ya kulinda biashara huria za ulimwengu na mfumo wa pande nyingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako