• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Mamlaka ya biashara kuchunguzwa

    (GMT+08:00) 2018-07-05 20:12:22

    Siku moja baada ya kuenguliwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amezitaka mamlaka za biashara kuacha urasimu kwa wafanyabiashara ili asitumbuliwe.

    Alitoa kauli hiyo jana wakati akizindua kliniki ya biashara inayolenga kutatua changamoto za kibiashara zinazowakabili wafanyabiashara na kukuza maendeleo ya viwanda na uwekezaji kwa wafanyabiashara wazawa.

    Amesema umefika wakati wa kutumia kliniki ya biashara huku kila mmoja akisimamia jukumu lake ili kuhakikisha wafanyabiashara wanafanikiwa na kukuza sekta ya viwanda na biashara.

    Alisema ikitokea mamlaka moja imefanya vibaya hata kama nyingine itafanya vizuri, wote wataonekana wabaya.

    Alishauri kila mamlaka isimamie jukumu lake kabla hazijashughulikiwa na kutaka kusiwapo na kesi za kuanzisha biashara kisha inakufa.

    Pia, alizitaka mamlaka hizo kutoa huduma za haraka kwa wafanyabiashara wanaotaka kujenga viwanda na kuwekeza washughulikiwe haraka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako