• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Gor Mahia Yazinduka na kuipiga Ports 2-0

  (GMT+08:00) 2018-07-06 08:31:49
  Mechi za mwisho za hatua ya makundi za kombe la Kagame zimechezwa usiku wa jana kwenye viwanja viwili vya Taifa na Azam jijini Dar es salaam.

  Ikicheza mechi yake ya kundi B, Gor Mahia ya Kenya imeifunga AS Ports ya Djibouti kwa mabao 2-0 na kumaliza jinamizi la sare lililokuwa likiwaandama.

  Kwenye mchezo mwingine uliochezwa Chamazi, Rayon Sports ya Rwanda imeisambaratisha Lydia Ludic ya Burundi kwa goli 3-1.

  Timu 8 zimefuzu hatua ya robo fainali ya michuano hii kutoka kundi A ni Azam fc ya Tanzania, Vipers ya Uganda na JKU ya Zanzibar. Kundi B, ni Rayon Sports ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya na AS Ports ya Djibouti. Na kundi C zipo Simba na Singida United za Tanzania.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako