Mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani unageuka kuwa vita ya kibiashara. Katika miezi mitatu iliyopita, kwa mara kadhaa Marekani imetishia kuongezaushuru wa forodha dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya mabilioni ya dola za kimarekani na hata mamia ya mabilioni, kwa kisingizio cha "Uvamizi wa kiuchumi wa China".
Mkurugenzi wa kamati ya biashara ya ikulu ya Marekani Bw. Peter Navarrohivi karibuni alitoa ripoti kuhusu "Uvamizi ya kiuchumi wa China watishia teknolojia na hakimiliki za Marekani na dunia", na kuanzisha rasmi kisingizio hiki kipya. Lakini kwa mujibu wa vigezo vya inachokiita "uvamizi wa kiuchumi" vilivyowekwa na Marekani yenyewe, Marekani imevamia karibu nchi zote duniani. Ili kulinda maslahi yake, Marekani imeanzisha vita vya kibiashara dhidi ya nchi mbalimbali bila kujali wenzi au maadui, nchi zilizoendelea au zinazoendelea. Kwa mfano Marekani imezilazimisha nchi za Afrika zikiwemo Rwanda, Kenya, Tanzania na Uganda kuacha au kupunguza ushuru wa forodha kwa nguo mitumba kutoka Marekani, ama sivyo zitaadhibiwa.
Madhumuni ya China ya kufanya ushirikiano na nchi nyingine ni kupata mafanikio ya pamoja. Katika kongamano la tatu la uwekezaji barani Afrika lililofanyika mwaka jana nchini Senegal, rais Macky Sall wa nchi hiyo alisema Afrika imepata fursa nzuri ya kujiendeleza kutokana na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na China.
Marekani haitaacha vitendo vya kulinda maslahi, na kuzuia maendeleo ya China katika muda mrefu, lakini China haitarudi nyuma kutokana na shinikizo la nje, na itaendelea kutoa mchango zaidi kwa dunia nzima.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |