• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa Zanzibar waonyesha dalili za kuimarika

    (GMT+08:00) 2018-07-06 19:10:43

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa Zanzibar iko vizuri katika ukusanyaji wa mapato, hatua ambayo imefanya uchumi wake uendelee kuimarika siku hadi siku.

    Aliyasema hayo alipokutana na uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakati ilipowasilisha utekelezaji wa Mpango Kazi wa Mwaka 2017/2018 na Mpango Kazi wa Utekelezaji kwa mwaka 2018/2019.

    Alipongeza uongozi huo pamoja na watendaji wake wote, kwa juhudi kubwa za ukusanyaji wa mapato na kueleza matumaini yake makubwa aliyonayo kwa wizara hiyo.

    Amesisitiza haja kwa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kutoa taarifa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari wakati changamoto zinapojitokeza katika utoaji wa huduma zake za fedha.

    Alisema ikilinganishwa na miaka ya nyuma, kwa kiasi kikubwa Zanzibar imepunguza kuwatumia wataalamu wa nje katika kuendesha miradi yake ya maendeleo na kazi nyingi katika wizara za serikali hivi sasa zimekuwa zikifanywa na wataalamu wazalendo, hali inayoonesha tofauti kubwa na nchi nyingi za bara la Afrika.

    Ametoa mwito kwa Wizara ya Fedha na Mipango kutonyamaza kimya kwani mapato ya Zanzibar yameimarika hivyo, ipo haja kwa wananchi kuyajua mafanikio hayo sambamba na mikakati iliyowekwa na serikali katika kuhakikisha mapato yake yanaimarika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako