• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakazi wa vijijini Tanzania kunufaika na umeme wa jua

    (GMT+08:00) 2018-07-06 19:11:25

    Kampuni ya Trend Solar inayotoa huduma ya umeme wa kulipia usiotegemea gridi imezindua uuzaji wa umeme wa jua nchini Tanzania utakaosaidia wanaoishi vijijini kuondokana na matumizi ya mishumaa na vibatari.

    Kampuni hiyo iliyoanza kutoa huduma mwaka 2017 imelenga kuwaleta watu wa vijijini katika ulimwengu wa kidigitali.

    Akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Trend Solar, Irfan Mizra amesema katika kuzingatia vipato vya watanzania wateja wanapewa nafasi ya kulipia kidogo kidogo hadi watakapokamilisha malipo.

    Ameongeza kuwa mteja ana uhuru wa kulipa hadi kwa muda wa miezi 18, wakati anaanza atalipia Sh139, 999 na kupewa huduma zote na ataendelea kulipia Sh17, 999 kila wiki ndani wiki ya 78.

    Amesema mteja anaponunua mashine za umeme wa jua, hupewa luninga ya kisasa ya inchi 24 ya kampuni ya Star Times, simu ya smati 4g ya kampuni hiyo na chaja yake, tochi ya kuchaji, betri ya smati sola, taa nne aina ya Led na dishi la Star Times.

    Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Sarah Cooke amesema watanzania wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo ili kupata maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako