• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya miongoni mwa nchi zinazotarajiwa kupata watalii wengi kutoka China

    (GMT+08:00) 2018-07-06 19:11:49

    Kenya ni miongoni mwa nchi 10 za Afrika ambazo zinatarajiwa kunufaika na watalii kutoka China.Kwa mujibu wa shirika la kukadiria uwezo wa kiuchumi Moody hali hiyo inatokana na ongezeko la asimilia 30 la watalii wanaoingia barani Afrika tangu mwaka wa 2012 kufuatia kuongezeka kwa mapato katika nchi hiyo.Nchi zingine ambazo zinatarajiwa kunufaika na idadi ya watalii kutoka China ni pamoja na Tanzania, Afrika Kusini, Mauritius, Namibia,Cape Verde ,Botswana na Tunisia. Hata hivyo idadi ya watlii wa China barani Afrika bado iko chini. Moody pia imesema kuwa kuongezeka kwa ndege za moja kwa moja kati ya miji mingi ya Afrika na China na hatua ya nchi za Afrika kurahisisha utaratibu wa kupata viza kutachangia zaidi ongezeko la idadi ya watalii wanaoingia barani Afrika. Hivi majuzi kampuni ya ndege ya Southern China iliongeza safari zake za moja kwa moja kati ya mji wa Nairobi na mji wa Guanzhou kutoka mbili. Mwaka jana shirika la ndege la Kenya lilisainia mapatano na shirika la ndege la Hong Kong kuongeza safari za ndege kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako