• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China ina imani na uwezo imara wa kulinda uchumi wake kuendelea vizuri kukabiliwa na vita ya kibiashara inayozushwa na Marekani

    (GMT+08:00) 2018-07-07 12:08:18

    Marekani jana imeongeza rasmi ushuru wa asilimia 25 dhidi ya bidhaa za bilioni 34 za kimarekani kutoka China, na kuzusha vita kubwa zaidi ya kibiashara katika historia ya kiuchumi. Wataalamu wa China wanaona, hatua hii ya Marekani ya kutumia ushuru kuwa ni zana iliyopitwa na wakati na inaonesha msimamo wake wa kudhalilisha wengine kibiashara, na China ina imani na uwezo imara wa kulinda uchumi wake kuendelea vizuri.

    Mtafiti wa kwanza katika kituo cha mawasiliano ya mambo ya uchumi wa kimataifa cha China Bw. Zhang Yansheng anaona, kampuni za Marekani ziko juu zaidi katika thamani ya mnyororo kuzilazimisha kampuni zao kurudi nchini Marekani kwa kupitia vita ya kibiashara, hatua hii yenyewe inasababisha utandawazi kurudi nyuma, na haitafanikiwa.

    "Kampuni zinapaswa kufuata kanuni za uchumi, kwa upande huu, binafsi naona kuwa, Marekani kuzusha vita ya kibiashara, halitatimiza lengo la kwenda kinyume na utandawazi na wala haitafanikiwa kuvunja mfumo wa mnyororo wa ugavi duniani. Sasa mnyororo wa thamani unaelekea mahitaji, China ina watumiaji wengi zaidi duniani wenye mapato ya kiwango cha kati, ina soko kubwa, ina mfumo kamili wa kiviwanda chain, pia ina mitaji mingi mikubwa". Naibu mkuu wa taasisi ya mambo ya China Bw. Jiyao anachambua kuwa, China imekuwa nchi ya pili kwa ukubwa kiuchumi duniani, China ina imani na uwezo kushinda msimamo wa Marekani wa kudhalilisha wengine kibiashara.

    "Tuna soko kubwa nchini, hivi sasa ukubwa wa soko la rejareja nchini umefika dola za kimarekani bilioni 6,000, ambao sio unaendana na ule wa Marekani, hata unatarajiwa kupita Marekani mwaka huu. Kwa upande wa kiviwanda, baada ya mabadiliko na maboresho ya kiviwanda miaka hii ya karibuni, muundo wetu wa kiviwanda unaboreshwa hatua kwa hatua, kusaidia viwanda nchini zimekamilishwa, vilevile utandawazi wa viwanda na miji uko njiani, ambao unakabiliwa na fursa nyingine za kukua zaidi. Hivyo soko letu la ndani, uwezo wetu wa uchumi, maendeleo ya kiwango cha teknolojia za viwanda, mahitaji makubwa katika sokozote hizo zinaunga mkono sana ukuaji wa uchumi wa China, pia ndiyo sababu tuna imani ya kushinda msimamo wa Marekani wa kudhalilisha wengine kibiashara, na kulinda imara uchumi wetu kuendelea enedelevu vizuri."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako