• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, CAF yawafungia waamuzi kuchezesha soka

    (GMT+08:00) 2018-07-09 10:33:45

    Kamati ya nidhamu ya shirikisho la kandanda barani Afrika (CAF) imetangaza kuwafungia waamuzi kutoka mataifa mbalimbali kutokana na makosa ya kinidhamu.

    Baadhi ya waamuzi waliofungiwa ni Jallow Ebrima kutoka Gambia na Yanissou Bebou kutoka Togo ambao wamefungiwa kujihusisha na soka kwa miaka kumi wakati mwamuzi msaidizi kutoka Kenya Aden Marwa amefungiwa maisha kujihusisha na masuala ya soka yanayosimamiwa na CAF.

    Uamuzi huo umetangazwa jana baada ya kikao cha kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo.

    Mwezi uliopita Marwa alituhumiwa kupokea rushwa na hivyo kuondolewa katika orodha ya waamuzi wasaidizi walioteuliwa kuchezesha fainali za Kombe la dunia nchini Urusi.

    Aidha waamuzi wengine wanaendelea kuchunguzwa na hatua zitachukuliwa baada ya kuitwa kwenye kamati ya nidhamu.

    Waamuzi wengine waliofungiwa ni:

    Boukari Ouedraogo, mwamuzi wa kati (Burkina Faso), Denis Dembele, mwamuzi wa kati (Cote d'Ivoire): Marius Tan, mwamuzi msaidiz (Cote d'Ivoire), Bi Valere Gouho, mwamuzi msaidizi (Cote d'Ivoire),Coulibay Abou, Rmwamuzi wa kati (Cote d'Ivoire), Jallow Ebrima, mwamuzi msaidizi (Gambia),

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako