• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirikisho la riadha Nigeria lafuta mashindano baada ya wanamichezo kugoma

    (GMT+08:00) 2018-07-09 10:37:53

    Shirikisho la mchezo wa riadha nchini Nigeria AFN, jana limefuta mashindano ya ubingwa wa kitaifa ambayo yalikuwa yanatarajiwa kufanyika mjini Abuja, kutokana na mgomo wa wanariadha kutokana na maandalizi yasiyoridhisha.

    Wanariadha hao ambao walionyesha kugoma kwa kukusanyika pamoja bila kufanya chochote uwanjani hapo, wakipaza sauti za kutaka kukutana na uongozi wa bodi ya AFN, ili kueleza matatizo yao ikiwemo kuecheleweshwa kwa malipo ya stahili zao na maandalizi mabovu kila mara wakati wa mashindano.

    Jambo lingine walilolalamikia ni kuhusu, mwakilishi wa wanariadha kwenye bodi ya AFN, wakitaka aondolewe kwa madai kwamba ameshindwa kuwasilisha matatizo hayo kwa ajili ya ufumbuzi.

    Baada ya tukio hilo la mgomo, Bodi ya AFN ilifanya mkutano wa dharura na kuyafuta mashindano hayo.

    Mashindano hayo pia, yalikuwa ni maalum kwa ajili ya kuandaa timu ya Nigeria itakayoshiriki mashindano ya Afrika mwezi ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako