• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tennis, Hatua ya 16 bora ya Wimbledon: Mechi kuchezwa leo mjini London

  (GMT+08:00) 2018-07-09 10:39:00

  Wachezaji Nyota wa mchezo wa Tennis duniani, Serena Williams wa Marekani, Roger Federer wa Uswisi na Rafael Nadal wa Hispania leo watacheza mechi dhidi ya wapinzani wao kwenye hatua ya 16 bora katika michuano ya Wimbledon inayoendelea mjini London nchini Uingereza.

  Bingwa mtetezi wa michuano hiyo kwa upande wa wanaume, Federer atacheza na Adriano Mannarino wa Ufaransa, ilihali bingwa mara tatu katika historia ya michuano hiyo Novak Djokovic anatarajiwa kucheza na Karen Kachanov wa Urusi.

  Kwa upande nyota namba moja kwa viwango vya ubora duniani kwa sasa, Rafael Nadal, yeye atacheza na Jiri Versley kutoka Jamhuri ya Czech.

  Kwa upande wa wanawake, mechi zinazotazamiwa kuwa ngumu zaidi, moja ni kati ya Serena Williams dhidi ya Evgeniya Rodina wa Urusi, na Angelique Kerber wa Ujerumani akitarajiwa kucheza na Belinda Bencic wa Uswisi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako