• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mashindano ya Magari ya Mwendokasi: Sebastian Vettel ashinda mbio za Uingereza

  (GMT+08:00) 2018-07-09 10:40:21

  Dereva Sebastian Vettel wa Ujerumani na timu ya Ferari jana ameibuka mshindi wa kwanza wa mashindano ya mbio za magari ya mwendokasi za Uingereza, jambo ambalo linamfanya kuwa wa kwanza kwenye msimamo wa viwango dhidi ya madereva wenzake msimu.

  Huu ni ushindi wa nne kwa Vettel kati ya mbio kumi ambazo zimekwisha kufanyika hadi sasa kwa mwaka huu, na kumfanya afikishe alama 171 ambazo ni faida kuelekea ubingwa wa jumla kwa mwaka huu.

  Mshindi wa pili kwenye mbio zilizofanyika mjini Northampshire alikuwa mwingereza Lewis Hamilton wa timu ya Mercedes na mshindi wa tatu akiibuka Kimi Raikonnen wa Finland na timu ya Ferrari.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako