• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa Kenya, Uganda unategemea kilimo kukua

    (GMT+08:00) 2018-07-09 20:23:55
    Uchumi wa Kenya na Uganda katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu, imeongezeka kwa asilimia 10 kutoka 2017.

    Kenya imesema uchumi wake uliongezeka kwa asilimia 5.7 katika miezi mitatu ya kwanza ya 2018, ikilinganishwa na asilimia 4.5 katika kipindi kama hicho mwaka jana.

    Uchumi wa Uganda kwa upande wake iliongezeka kwa asilimia 6.4, kutoka asilimia 4.5 kutoka kipindi kama hicho mwaka jana, hii, inatokana na kilimo ambacho kiliandika ukuaji wa asilimia 6.6.

    Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS) imesema kuwa sekta ya kilimo iliongezeka kwa asilimia 5.2 katika robo ya kwanza, ikilinganishwa na asilimia moja katika kipindi hicho mwaka jana.

    Kenya sasa inatarajia kukua kwa asilimia 5.8 mwaka huu, kutoka asilimia 4.9 mwaka 2017.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako