• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Balozi wa China katika UN atoa wito kuwalinda watoto walioko kwenye mapambano

  (GMT+08:00) 2018-07-10 09:37:48

  Balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw Ma Zhaoxu ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kufanya juhudi kuwalinda watoto walioko katika mapambano.

  Amesema kipaumbele kinapaswa kutolewa katika kuwaelimisha watoto wathamini amani na kupinga vita, ili kuwakinga dhidi ya madhara ya ugaidi na itikadi kali. Jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuchukua hatua zenye ufanisi kupambana na uandikishaji wa watoto kwenye makundi ya kigaidi, pamoja na kuchochea vurugu na kueneza itikadi kali kupitia mtandao wa internet.

  Balozi Ma ameongeza kuwa njia yenye ufanisi zaidi katika kuwalinda watoto ni kuzuia na kutatua mapambano. Amesema baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linapaswa kuhimiza matumizi wa mbinu za kisiasa katika kuitatua migogoro kwa njia ya amani, na kuzuia mapambano ya kisilaha yasitokee.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako