• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanariadha 64 waanza kambi ya maandalizi

  (GMT+08:00) 2018-07-10 10:08:29

  Nyota wawili kwenye mchezo wa riadha nchini Kenya, Mike Mokamba na Fresha Mwangi wamejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kitakachokwenda kushiriki mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kuanza Agosti Mosi mjini Asaba nchini Nigeria.

  Mokamba atashiriki mbio za mita 200 na mbio za kupokezana vijiti za mita 100, nah ii itakuwa ni mara yake ya pili baada ya kufanya hivyo tena mwaka 2016 katika mashindano kama hayo nchini Afrika Kusini.

  Lakini Fresha Mwangi, anatarajiwa kushiriki mbio za mita 100, na mbio za kupokezana vijiti za mita 100.

  Jumla ya wanariadha 64 wameanza kambi kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako