• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Luis Enrique ateuliwa kuwa Kocha wa timu ya taifa ya Hispania

  (GMT+08:00) 2018-07-10 10:12:32

  Kocha mkuu wa zamani Barcelona, Luis Enrique ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa ya Hispania ikiwa ni siku chache baada ya timu hiyo kuondolewa katika fainali za Kombe la dunia.

  Enrique anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Fernando Hierro ambaye alijiuzulu baada ya kuiongoza timu hiyo kwa siku 25 tu tena kwa dharura ikiwa kwenye kombe la dunia.

  Katika hatua nyingine, Shirikisho la soka la Hispania limemtangaza golikipa wa zamani wa Atletico Madrid Jose Francisco Molina kuwa mkurugenzi wa ufundi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako