• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China afanya mazungumzo na mfalme wa Kuwait

  (GMT+08:00) 2018-07-10 10:28:18
  Rais Xi Jinping wa China amekutana na mfalme wa Kuwait Sabah Al-Ahmed Al-Jaber Al-Sabah ambaye yuko ziarani nchini China.
  Kwenye mazungumzo yao marais hao wameamua kuanzisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Kuwait, ili kutia nguvu mpya na kufungua mustakabali mpya kwenye uhusiano wa nchi hizo mbili katika zama mpya.
  Rais Xi amesema China inapenda kuimarisha mawasiliano na uratibu na Kuwait na kuendelea kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati yake na Kamati ya Ushirikiano wa Nchi za Ghuba na kuhimiza amani na utulivu wa kikanda kwa pamoja.
  Kwa upande wake Mfalme Sabah amesema chini ya msingi wa kuaminiana, Kuwait inapenda kuimarisha ushirikiano na China kwenye nyanja mbalimbali, haswa kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia moja", ili kuhimiza kwa pamoja amani na usalama katika kanda ya Ghuba na dunia nzima.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako