• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa nane wa ngazi ya mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu waanza Beijing

    (GMT+08:00) 2018-07-10 10:48:01

    Mkutano wa nane wa ngazi ya mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu umeanza leo hapa Beijing, na kuhudhuriwa na rais Xi Jinping wa China, mfalme wa Kuwait Sheikh Al-Sabah ambaye yuko ziarani nchini China, mawaziri wa nchi 21 za kiarabu na katibu mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu AL Ahmed Aboul-Gheit.

    Rais Xi Jinping wa China anatarajiwa kutoa hotuba muhimu, akieleza maoni ya China kuhusu kuimarisha usanifu wa ngazi ya uongozi wa kukuza uhusiano kati ya China na nchi za kiarabu, kupanga ushirikiano, na kulijenga Baraza hilo. Pia atatoa pendekezo muhimu kwa China na nchi za kiarabu kuimarisha ushirikiano kwenye mpango wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kueleza "mpango wa China" katika masuala yanayolikabili eneo la Mashariki ya Kati kulingana na mahitaji ya pande mbalimbali.

    Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu lilizinduliwa mwaka 2004 na linalenga kuimarisha mawasiliano, ushirikiano kati ya pande hizo mbili na pia kuhimiza amani na maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako