• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ushirikiano kati ya China na nchi za kiarabu waleta ustawi

  (GMT+08:00) 2018-07-10 19:22:32

  Mkutano wa 8 wa ngazi ya mawaziri wa baraza la ushirikiano kati ya China na nchi za kiarabu umefanyika leo hapa Beijing.

  Katika miaka ya hivi karibuni uhusiano kati ya pande hizo mbili umekuwa mzuri siku hadi siku, kwani China imefuata kanuni ya kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, na kusisitiza kutatua mgogoro kwa njia ya mazungumzo.

  Mwezi Januari mwaka jana, Rais Xi Jinping wa China alipozungumza kwenye mkutano wa kilele wa Davos alisisitiza kuwa, sababu ya China kugeuka kuwa nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi kutoka nchi maskini si uvamizi na ukoloni, bali ni kufanya kazi kwa bidii na kulinda amani. China inatetea mazungumzo badala ya mvutano katika suala la Mashariki ya Kati, na kuunga mkono nchi za Afrika kuungana na kushikamana.

  Hivi sasa kutokana na mabadiliko ya hali ya kimataifa, China na nchi za kiarabu zinapaswa kuongeza zaidi mawasiliano na ushirikiano, ili kuanzisha mustakabali mzuri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako