• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Mataifa wazingatia utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu

  (GMT+08:00) 2018-07-10 19:52:53

  Mkutano wa kisiasa kuhusu maendeleo endelevu wa Umoja wa Mataifa umefunguliwa jana katika makao makuu ya umoja huo mjini New York, na utajadili mchakato wa utekelezaji wa nchi 47 wa malengo ya maendeleo endelevu.

  Akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano huo wa siku nane, naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshugulikia uchumi na jamii Bw. Liu Zhenmin amesema, ingawa mafanikio kadhaa yamepatikana katika siku za karibuni, lakini, bado kuna matatizo mengi, kama vile, ongezeko la watu wanaokabiliwa na njaa, ukosefu wa huduma za afya, maji safi na salama, uharibifu wa mazingira kutokana na maendeleo, ongezeko la joto duniani, mabadiliko ya hali ya hewa na ongezeko la migogoro.

  Mwenyekiti wa baraza la uchumi na jamii la Umoja wa Mataifa Bibi Marie Chatardova amesema, malengo hayo yatatimizwa si kama tu kwa mchango wa nchi mbalimbali bali pia yanahitaji jitihada za mashirika ya jamii, sekta binafsi na taasisi maalum.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako