• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar: Zanzibar yafunga ofisi ya usajili wa meli Dubai

    (GMT+08:00) 2018-07-10 19:56:08
    Zanzibar imefunga ofisi ya usajili wa meli huko Dubai katika Falme za Kiarabu, ili kudhibiti biashara ya bidhaa haramu.

    Hatua hiyo inakuja miezi sita baada ya Rais John Magufuli kuamuru kupigwa marufuku usajili wa meli za kigeni nchini Tanzania na kuagiza kukaguliwa kwa meli 470, baada ya ripoti kuibuka kwamba meli kadhaa za zenye bendera ya Tanzania zilihusika na biashara haramu ya silaha na madawa ya kulevya.

    Waziri wa Zanzibar wa Miundombinu, Usafiri na Mawasiliano Dr Sira Ubwa Mamboya alisema kuwa kukamatwa kwa meli za kigeni zenye bendera ya Tanzania na ambazo zinabeba madawa ya kulevya na silaha kuliathiri biashara ya bahari katika kisiwa hicho.

    Zanzibar awali imelaumiwa kwa kuruhusu meli za Irani na Korea Kaskazini zinazotumia bendera ya Tanzania ili kuepuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa vinavyowekwa katika nchi hizo mbili kutokana na tuhuma za miradi yao ya nyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako