• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Shoprite yaingia majumba ambayo awali yalikuwa na maduka ya Nakumatt

  (GMT+08:00) 2018-07-10 19:56:27
  Maduka ya Shoprite ya Afrika Kusini yameanza kuingia kwenye majumba ambayo awali yalikuwa na maduka ya Nakumatt mjini Kampala Uganda.

  Shoprite imekuwa na maduka mawili tu nchini Uganda tangu iingie nchini humo mwaka wa 2000.

  Nakumatt nayo ambayo imekuwa na maduka kadhaa katika kanda ya Afrika Mashariki, imeendelea kufunga matawi yake mengi kutokana na hasara kubwa.

  Katika kipindi cha miezi 6 Shoprite imechukua majumba matatu yaliokuwa na maduka ya Nakumatt yakiwemo Acacia Mall eneo la Kamwokya, Victoria Mall mjini Entebbe na Village Mall eneo la Bugolobi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako