• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Bima ya kilimo kuanzishwa Tanzania

  (GMT+08:00) 2018-07-10 19:57:08
  Shirika la Bima la Taifa Tanzania (NIC) litaanzisha na Bima ya Kilimo, itakayosaidia kuunga mkono jitihada za serikali za kujenga uchumi wa viwanda.

  Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Sam Kamanga amesema kilimo ndiyo uti wa mgongo wa taifa na ndicho kinachotoa malighafi nyingi za viwandani nchini, hivyo aina hiyo ya bima itasaidia kujenga uchumi wa viwanda.

  Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Maonesho ya 42 ya Sabasaba yanayoendelea Dar es Salaam katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, amesema NIC inaunga mkono jitihada za serikali za ujenga uchumi wa viwanda na kwamba aina hiyo ya bima itakuwa pia mkombozi wa wakulima pale majanga yanapowafika.

  Alisema shirika lake limeimarisha huduma yake ya bima ya magari kwa nchi za Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) ili kuondoa udanganyifu. Alisema huduma hiyo kwa sasa imewekwa katika mfumo wa kidijiti hali ambayo inazuia bima bandia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako