Taakwimu kutoka kwa halmashauri ya Chai nchini humo zinaonyesha chai iliozalishwa kati ya Januari na mwezi Mei ni kilo milioni 187 ikilinganishwa na kilo milioni 160 kipindi sana na hicho mwaka jana.
Ongezeko la uzalishaji limechangiwa na kuongezeka kwa mvua lakini pia nayo bei kwa kilo moja imeshuka hadi dola 28 ikilinganishwa na dola 29 mwaka jana.
Kenya huuza kwa wingi chai yake nchini Misri, Uingereza, Pakistan, Afghanistan, Iran, Sudan, Yemen na Milki za kiarabu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |